17 Oktoba 2014 - 07:11
Rais wa zamani wa C.I.A. atamani kuonana na kamanda Sulaimaniy

Rais wa zamani wa CIA ambaye pia alikuwa waziri ulinzi wa zamani wa Marekani amesema moja miungoni mwa matumaini yangu ni siku moja kuweza kuonana ana kwa ana na kamanda Qasim Sulaimaniy na kuzungumza naye.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Rais wa zamani wa CIA baada ya kukiri pigo kali waliolipata kutoka kwa jeshi la Quds la Iran katika uendeshaji wa mipangilio ya mapambano yake, jeshi la Quds ni jeshi ambapo liko chini ya jeshi la sepaha la Iran, Rais huyo wa zamni sasa matumai yake makubwa ni kuonana na kamanda wa jeshi hilo la Quds Jeneral Qasim Sulaimaniy.
(Leon Panetta) Rais wa zamani C.I.A na aliyekuwa waziri ulinzi wa zamani wa Marekani alipokuwa katika mahujiano na televishen ya  Bloomberg News kuhusu harakati za jeshi la Quds la Iran.
Naye katika mazungumzo yake alielezea matumaini yake ya kuonana na mkuu wa jeshi hilo jeneral Sulaimaniy, katika kujibu akijibu swali la mwendesha kipindi cha televishen hiyo ambaye alimuuliza je unapenda kuonana na kufahamiana na jeneral Sulaimaniy? Alisema kwakweli ninapaswa kusema kuwa mara kadhaa nimeshuhudia miundompinu mbali mbali ya maficho kutoka katika jeshi la Iran la Quds nikiwa sehemu mbalimbali.
Naye alindelea kusema napaswa kusema kwamba moja kati ya matumaini yangu makubwa ni kuonana uso kwa uso na kamanda Sulaimaniy nakupata kuzungumza naye hata kwa muda mchache.
Inasemekana kuwa kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kimarekani jenerali Qasim Sulaimaniy ndiye mwenye mchango mkubwa katika kulipatia nguvu jeshi la HizbullaLebanon, kudhibiti hali ya kisiasa ya Iraq baada ya kuporomoka utawala Sadamu Husein pia kubadilisha hali ya vita ya ndani nchini Syria.
Kamanda huyu mara kadhaa alishawahi tuhumiwa na utawala wa Marekani kwa kuingilia masuala ya Iraq, na katika mitazamo ya nchi za ulaya na Marekani yeye ni ndye mtu namba moja kwa koto pendwa pia  kusifiwa kwa harakati zake za kijeshi, ambapo John Maguire mwanajeshi wa zamani wa CIA nchini Iraq anasema: Qasim Sulaimaniy ndiye Jeneral mwenye uwezo kuliko majeneral wote katika mashariki ya kati katika uapangiliaji wa vita naye haonekani mara kwa mara na yeyote.
Ama katika jarida la kmarekani la (Wired) yeye yuko nmaba moja katika idadi ya watu hatari zaidi duniani, pia katika jarida The New Yorker la marekani, yeye ndiye kamanda aliyefanya mabadiriko makubwa katika vita ya ndani ya Syria.